UKWELI USEWME.

​UKWELI USEMWE💯%

Collian Andrew
Ebu tusidanganyane. Katika ulimwengu wa leo hakuna mjinga anayengoja kuerevuka maana kila mtu amepevuka. Hivyo basi walaghai wako taabani. Wapenda za bwerere hawana lao. 
Sitaki tuitane ndugu wala rafiki ili tuendelee kunyanyasana. 

Tusisengenyane. Tuyaweke mambo paruwanja, mchana mwangani, tukionana uso kwa macho. Tusije tukaanza kulaumiana au kulalamikiana na kuitana visivyosemeja. Tusemezane. Maana huku kufichaficha mambo ndiko chanzo haswa cha maovu yanayotanda duniani. Huku kunyamazia mambo ndiko kunawatuma maelfu ya  watu makaburini kabla ya wakati wao kutimia. Kwa nini usiseme yanayokuudhi? Kwa nini unyamazie fundo rohoni? 
Mtu anakukopa pesa kisha unaanza kumwadithia paukwa pakawa sisizo na mwisho. “Ningekuwa nazo….” Ya nini? Mwambie ukweli umuume! ” Ninazo lakini SI-KU-PI!” Mkumbushe mwaka jana alikukopa pesa aende  mashambani kwa shughuli zake mwenyewe akiahidi kurejesha pindi arudipo. Hakurejesha wala kuomba radhi. Alijisahulisha. Mwambie anakukera.
Mkumbushe tena miezi miwili iliyopita. Alikuomba fedha alipe kodi ya nyumba baada ya mshahara wake kucheleweshwa. Mnukulie maneno yake;  “tafadhali ndugu yangu nakuhakikishia… ” Muulize kama alikukumbuka tena pindi alipoupata huo mshahara. Muulize alikwenda wapi na kwa nini. 
Usimweke chini. Mwonyeshe vile anavyotumia pesa zake baada ya kuzipokea. Hakumbuki vya kesho; ala kama mchwa. Mhesabie kina Salome, Mwende na Nyamari. Wote ambao huwanunulia pizza katika mikahawa ya kifahari mjini kwa minajili ya kupaliwa sifa.
Hatimaye, mkumbushe ukimsizitia kuwa humpi. Usikubali mtu  kukuona daraja wakati wa mafuriko. Ongea vibaya waseme watavyosema. Ukweli usemwe na tuache kudanganyana!

Advertisements

6 thoughts on “UKWELI USEWME.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s